Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ndio Tuzo pekee ambayo Messi hajawahi kushinda

Lionel ,Messi Only Award Lionel Messi

Wed, 28 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa, Lionel Messi ameshinda karibu kila kitu kinachopaswa kushinda kwa zaidi ya miongo yake miwili aliyotamba kwenye soka.

Muargentina huyo alishinda Kombe la Dunia wiki iliyopita wakati alipoiongoza Argentina kubeba ubingwa huo huko Qatar. Na sasa ameshinda mataji 42 kwa klabu yake na timu ya taifa, amebakiza taji moja tu kuwa mchezaji aliyebeba mataji mengi zaidi duniani kwenye soka.

Kwenye tuzo binafsi, Messi ameshinda Ballon d’Or mara saba na amejiweka pazuri kwenye kushinda ya nane itakayotolewa 2023.

Ameshinda pia Kiatu cha Dhahabu cha Ulaya mara sita na amewahi kutajwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Fifa kwa upande wa wanaume mwaka 2019.

Lakini, kuna taji moja ambalo Messi hajabeba hadi sasa. Mguu wa Dhahabu.

Tuzo ya Mguu wa Dhahabu ilianza kutolewa mwaka 2003 na imekuwa ikitolewa kwa wanasoka bora duniani wenye umri unaozidi miaka 28. Washindi huchaguliwa na jopo la waandishi wa habari wa kimataifa, wakichangua mchezaji mmoja kwenye orodha ya wakali 10. Mchezaji anashinda tuzo hiyo mara moja tu.

Tuzo ya Mguu wa Dhahabu kwa mwaka 2022 ilitolewa Monaco Jumatano iliyopita na straika wa Barcelona na Poland, Robert Lewandowski ndiye aliyeibuka kinara.

Jambo hilo limemfanya Lewandowski kuungana na wakali wengine wenye majina makubwa kwenye soka ambao waliwahi kushinda tuzo hiyo kwa miaka 20 iliyopita.

Messi, 35, bado hajawahi kushinda tuzo hiyo licha ya umahiri wake alioinyesha kwenye soka kwa miaka saba iliyopita ambayo inamfanya kuwamo kwenye vigezo. Kwa mwakani anaweza kuwa kwenye ushindani mkali wa kubeba tuzo hiyo sambamba na Karim Benzema, Kevin De Bruyne na Virgil van Dijk - miongoni kwa wenye vigezo vinavyotakiwa.

Mastaa waliowahi kushinda Mguu wa Dhahabu

2003: Roberto Baggio 2004: Pavel Nedved 2005: Andriy Shevchenko 2006: Ronaldo 2007: Alessandro Del Piero 2008: Roberto Carlos 2009: Ronaldinho 2010: Francesco Totti 2011: Ryan Giggs 2012: Zlatan Ibrahimovic 2013: Didier Drogba 2014: Andres Iniesta 2015: Samuel Eto’o 2016: Gianluigi Buffon 2017: Iker Casillas 2018: Edinson Cavani 2019: Luka Modric 2020: Cristiano Ronaldo 2021: Mohamed Salah 2022: Robert Lewandowski

Chanzo: www.tanzaniaweb.live