Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Willy Onana amefungukia ukaribu wake na Kocha Mkuu Roberto Oliviera 'Robertinho' kuwa ulianza walipokutana kwenye mechi ya kirafiki.
Akifanya mahojiano na Simba APP, Onana alisema, akiwa anaitumikia Rayon Sports ya Rwanda, walikutana na Vipers iliyokuwa inanolewa na Robertinho katika mechi ya kirafiki na tangu hapo mwalimu alianza kumfuatilia.
"Siku hiyo nilikiwasha sana nikawasumbua sana mabeki wa Vipers hivyo kutokea pale mwalimu aliendelea kunifuatilia hadi nikatua Simba," alisema Onana raia wa Cameroon.
Onana alikuwa na msimu mzuri na Rayon ambapo msimu uliopita alikuwa MVP wa Ligi Kuu kabla ya kutua Msimbazi kwa ajili ya msimu mpya wa 2023-24.