Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii hapa rekodi za Yanga Ligi ya Mabingwa

Yanga Kimataifa Kikosi cha Yanga

Thu, 29 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wakielekea kwenye wiki ya Kimataifa, wiki ambayo mashabiki na wanachama wa Yanga wana ndoto kubwa ambayo tumesubiria kwa miaka mingi.

klabu ya Yanga imesema malengo yao makubwa ya Kutinga hatua ya makundi kwa mara nyingine ili kuenzi kile kilichofanywa na malegend wao mwaka 1998.

Yanga ndio timu ya kwanza kufuzu makundi ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza kutoka Tanzania ambapo walifanya hivyo mwaka 1998, na kuweka rekodi nyingine ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza mwaka 2018.

Mchezo wao wa kwanza utachezwa Tarehe 8-10-2022 Uwanja wa Benjamini Mkapa Muda saa 10 jioni.

Mchezo wao wa marejeano utachezwa Tarehe 16-10-2022 Uwanja wa Al Hilal Omduraman Sudan

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Yanga kwenda Sudan katika michuano ya Ligi ya Mabingwa baada ya kufanya hivyo mnamo Mei 1973 ambapo Yanga walitoka sare ya 1-1 dhidi ya El Merriekh.

Takwimu muhimu za Kuzingatia

Mpaka kufikia hivi sasa Yanga imecheza michezo 89 ya Ligi ya Mabingwa Ushindi – 29 Sare – 30 Kupoteza – 30.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live