Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii hapa ratiba ya micheo ya Leo Ligi Kuu Bara

Ratiba Leo 6 Ratiba michezo ya Ligi Kuu NBC, Februari 6

Sun, 6 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Primia Ligi) 2021/2022 inaendea leo kwa michezo mitatu katika viwanja tofauti ikiwa ni raundi ya 15 hivi sasa.

Mchezo wa kwanza utapigwa kule katika uwanja wa Nyankumbu- Geita ambapo wenyeji Geita Gold FC, wataikaribisha Timu ya Polisi Tanzania majira ya saa kumi jioni.

Katika Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi wenyeji Namungo FC wataikaribisha Mtibwa Sugar FC.

Mchezo unaosubiriwa kwa hamu ni ule utakaopigwa katika dimba la Mkapa majira ya saa moja usiku ambapo Simba SC, watavaana na Mbeya Kwanza.

Ligi Kuu Bara inaongozwa na Yanga wenye alama 36 kileleni wakifuatiwa na Simba wenye alama 28 huku Azam akikamata nafasi ya tatu wakiwa na alama 25.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live