Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii hapa mashine mpya ya Dodoma Jiji FC

Apollo Otieno Onyango Apollo Otieno Onyango

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Uongozi wa Dodoma Jiji FC umemtambulisha kiungo mpya ambaye ni Apollo Otieno Onyango ambaye amejiunga nao akitokea KCB ya Kenya kwa mkataba wa miaka miwili.

Ofisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga amesema: “Ni kweli tumemsajili atakuja kutuongezea nguvu eneo la kiungo, atakuwa sambamba na Mtenje na Gustapha hivyo natumaini watatupa kile ambacho Apollo anacho, maana wana uzoefu na ligi.

“Malengo yetu mzunguko wa pili wa 2023/2024 ni kuweza kumaliza nafasi za nne za juu ukiangalia msimu uliopita hatukuweza kufika malengo yetu na sasa tunasajili wachezaji bora na wenye uzoefu mkubwa ili kuweza kuleta matokeo chanya kwenye mpira wetu wa sasa.”

Mbali na nyota huyo, pia Dodoma walitangaza kumrudimba kundini Mshambuliaji Anuary Jabir.

Chanzo: Dar24