Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii hapa hatma ya timu za majeshi Ligi Kuu

Polisi Tanzania Hali Tete.jpeg Hii hapa hatma ya timu za majeshi Ligi Kuu

Fri, 5 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaelekea ukingoni kwa msimu huu wa 2022/23, hali na mwenendo wa timu za majeshi Polisi Tanzania ya Moshi mkoani Kilimanjaro na Ruvu Shooting ya Pwani, inazidi kuwa mbaya.

Katika msimamo wa Ligi hiyo Polisi Tanzania inashika nafasi ya 15 ikiwa na alama 22 walizokusanya kwenye michezo 27 ikifuatiwa na Ruvu Shooting ambao wapo nafasi ya mwisho wakiwa na alama 20 zote zimecheza michezo 27.

Kikosi cha Polisi Tanzania ambacho kwa sasa kipo chini ya Kocha kutoka DR Congo Mwinyi Zahera, kimefanikiwa kushinda michezo mitano, huku kikipata sare saba na kupoteza mara 15.

Ruvu Shooting nao wameshinda michez mitano, wakipata sare tano na kupoteza mara 17. Timu hizi mbili zimebaki na michezo mitatu tu ambayo itaamua hatma yao katika mashindano ya ligi msimu huu wa 2022/23.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: