Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii hapa droo mpya hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa

Re Draw Hatua ya 16 bora haitawakutanisha tena Messi na Ronaldo

Mon, 13 Dec 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Droo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora imekamilika huku stori kubwa ni kupangua ratiba ya awali ambayo ingewakutanisha wakali wawili wa soka duniani Cristiano Ronaldo na mpinzani wake Lionel Messi.

Manchester United ilipangwa kucheza na Paris Saint-Germain hatua ya mtoano ambayo lakini baadae ikaja kujulikana kulikuwa na tatizo la kimitambo.

Baada ya kurudia kupanga ratiba hiyo Manchester United atacheza na Atletico Madrid huku PSG akisakatana na Real Madrid.

Chelsea itamenyana na Lille ya Ufaransa huku Liverpool ikionyeshana umwamba na Inter Millan ya nchini Italia.

Kwa upande wa Manchester City imepangiwa kucheza dhidi ya Sporting CP ambayo ataanzia kucheza ugenini.

Bayern Munich wao itakuwa na kibarua hidi ya RB Salzburg, Ajax itacheza dhidi ya Benfica, Villarreal itakuwa nyumbani kumenyana na Juventus.

Mechi zote za mtoano za Ligi ya Mabingwa Ulaya, zitaanza kuchezwa kuanzia  tarehe Februari 15 na 14 mwakani.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz