Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii hapa Droo ya hatua ya 16 Bora UEFA

HHLNCCvo.jpeg Hii hapa Droo ya hatua ya 16 Bora UEFA

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Droo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika imetoka ambapo vigogo 16 waliofuzu hatua hiyo wakibaini wapinzani wao.

Vigogo wa London, Arsenal wamepangwa dhidi ya miamba ya Ureno FC Porto huku Mabingwa watetezi, Manchester City wakipangwa dhidi ya wababe wa Manchester United, FC Copenhagen.

Mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo, Real Madrid wamepangwa dhidi ya vigogo wa Ujerumani, RB Leipzig huku FC Barcelona ikikutanishwa na Mabingwa wa Italia, Napoli.

Inter Milan ya Italia imepewa mfupa mgumu baada ya kupangwa dhidi ya vigogo wa Uhispania, Atletico Madrid huku PSG ya Ufaransa ikipewa Real Sociedad ya Uhispania.

DROO KAMILI

Copenhagen vs Man City

RB Leipzig vs Real Madrid

Porto vs Arsenal

Napoli vs Barcelona

PSG vs Real Sociedad

Inter vs Atletico Madrid

PSV vs Dortmund

Lazio vs Bayern Munich

Chama lako limepangwa na nani?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live