Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii Liverpool, hakuna wa kuwazuia

Gakpo X Nunez Stood Hii Liverpool, hakuna wa kuwazuia

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pisha njia, gari la Liverpool breki imekatika, kaa mbele ugongwe. Ndicho unachoweza kusema kuhusu kiwango cha sasa cha miamba hiyo ya Anfield, gari sasa limewaka.

Chama hilo la Kocha Jurgen Klopp ndilo linaloshika usukani wa Ligi Kuu England kwa sasa, huku ikiwa kwenye kiwango bora kwelikweli kuzidi timu nyingi za Ulaya kwa wakati huu.

Liverpool ilikuwa ovyo sana msimu uliopita, lakini fasta sana baada ya miezi michache tu msimu huu, imerudi kwenye ubora wao na sasa haishikiki.

Kwa sasa inaongoza msimamo wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya pointi tano na haipo kwenye kilele hicho cha msimamo wa ligi hiyo kwa mashaka, wapo vizuri kwelikweli.

Ushindi wao wa mabao 4-0 katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Bournemouth ilionyesha walivyo siriazi msimu huu, huku ikipata matokeo hayo bila ya huduma ya wakali wake matata kama Mohamed Salah na Trent Alexander-Arnold.

“Kwa kipindi hiki tumejipata, tuna nguvu naweza kusema sasa tupo vizuri," alisema Klopp.

Liverpool imeonekana kupata njia bora ya namna ya kushinda mechi zake msimu huu na takwimu zake zimekuwa zikiwavutia mashabiki wao na kila mmoja kwa sasa amekuwa na raha.

Takwimu hizi zinathibitisha ubora wa kikosi hicho cha Anfield na bila ya shaka kitakuwa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England ikichuana na Manchester City na Arsenal zinazotajwa kuwapo kwenye vita hiyo.

1. Liverpool imevuna pointi 19 kutoka kwenye mechi ambazo hakika ilionekana kama inakwenda kupoteza kwa msimu huu. Kwa ligi nyingine kubwa za Ulaya ni Girona pekee ndiyo waliovuna pointi nyingi kwa staili hiyo kuwazidi Liverpool, pointi 22 huko kwenye La Liga.

2.Liverpool kwa sasa ina wastani wa kuvuna pointi 2.28 kwa kila mechi na hivyo kutabiriwa kumaliza msimu na pointi 87 kama itakwenda kwa mwendo huo hadi mwisho na zitakuwa pointi nyingi kwenye nne bora katika kipindi cha Kocha Klopp kuinoa timu hiyo.

3. Kikosi hicho cha Klopp kimepiga mashuti 388 kwenye ligi, ikiwa ni mengi kuzidi Ligi Kuu tano bora za Ulaya. Bayern Munich inashika namba mbili kwa kupiga mashuti 343.

4. Liverpool imepoka mipira kwa staili ya kulala yombo mara 61 kwenye eneo la timu pinzani, ikiwa ni rekodi inayoweza kufikiwa na timu za Tottenham Hotspur na PSG tu kwa msimu huu.

5. Miamba hiyo ya Merseyside imekuwa bora pia kwenye kurudisha mipira kwenye umiliki wake msimu huu. Ikirejesha mpira kwenye himaya yake mara 1,172 na kwa timu za kutoka ligi kubwa za Ulaya ni Athletic Bilbao pekee yao ndiyo yenye uwezo wa kushindana na Liverpool kwenye hilo msimu huu.

6. Liverpool bado haijapoteza mechi kwenye Ligi Kuu England msimu huu ilipotangulia kufunga bao. Na kinachovutia kwenye mechi hizo, ilishindwa kupata ushindi kwenye mechi mbili tu, ambazo yenyewe ilitangulia kufunga bao na mchezo ukamalizika kwa sare.

7. Klopp na kikosi chake ukicheza nao mechi haijaisha hadi iishe kabisa. Miamba hiyo imefanikiwa kufunga mabao saba kwenye dakika za majeruhi, ikiwa ni mengi zaidi kwa Ulaya, wakichuana na Arsenal.

8. Liverpool haijapoteza mechi kati ya 14 za mwisho kwenye Ligi Kuu England. Ni Juventus (mechi 16) na Bayer Leverkusen (mechi 18) pekee ndizo kwa sasa zimekuwa na rekodi ya kucheza mechi nyingi bila kutopoteza kwa kipindi hiki katika Ligi Kuu tano bora za Ulaya.

MECHI ZIJAZO ZA LIVERPOOL

-Januari 24 vs Fulham (EFL Cup, ugenini)

-Januari 28 vs Norwich (FA Cup, nyumbani)

-Januari 31 vs Chelsea (EPL, nyumbani)

-Februari 4 vs Arsenal (EPL, ugenini)

-Februari 10 vs Burnley (EPL, nyumbani)

-Februari 17 vs Brentford (EPL, ugenini)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live