Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Heshimu mpira usiseme Yanga watafungwa ugenini - Luambano

YANGA 4 7 Alex Luambano

Wed, 31 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa masuala ya soka wa Clouds FM, Alex Luambano amesema kuwa watu wanatakiwa waheshimu matokeo ya soka na si kuhukumu kuwa Yanga itafungwa ugenini na USM ALger katika mchezo wa marudiano.

Yanga atakuwa na kibarua kigumu mbele ya Waarabu hao Jumamosi ijayo nchini Algeria katika mchezo wa pili wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya mchezo wa kwanza kumalizika kwa Yanga kufungwa bao 2-1.

“Baada ya Yanga kupoteza mechi ya kwanza ya Fainali ya Komba la Shirikisho Afrika, wapo wanaouheshimu mchezo na wanazungumza kwa kuuheshimu mchezo lakini kuna watu hawauheshimu kabisa mchezo na hawawaheshimu wachezaji.

“Kwa matokeo iliyopata Yanga nyumbani [kupoteza 2-1] huwezi kusema tayari mchezo umekwisha na watafungwa kwenye mechi ya ugenini! Tuuheshimu mchezo wa mpira wa miguu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: