Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hesabu za Namungo hizi hapa

Namungoi Waichapa Azam FC Hesabu za Namungo hizi hapa

Wed, 31 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Namungo FC Dennis Kitambi amesema kuwa wanaimani kubwa ya kupata matokeo mazuri kwenye mchezo ujao wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji.

Timu ya Namungo mchezo wake uliopita ilishinda mbele ya Azam FC kwa mabao 2-1 mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Inatarajiwa kucheza na Dodoma Jiji, Juni 6 Uwanja wa Majaliwa ikiwa ni mzunguko wa pili.

“Tulipata matokeo mazuri mchezo uliopita ugenini hapo tunakwenda kufanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji ambao hautakuwa mwepesi.

“Kikubwa ni kufanyia kazi makosa kwenye mechi zetu zote kwani licha ya kupata ushindi bado kuna makosa ambayo yamekuwa yakifanyika kwa wachezaji hilo tutalifanyia kazi,”

Namungo imefikisha pointi 39 ikiwa nafasi ya tano kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 28.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: