Aliyekua kocha wa timu ya taifa ya Saudia Arabia Herve Renard amefanikiwa kuachana na timu hiyo na kwasasa atatimkia timu ya taifa ya wanawake ya Ufaransa na kuanza kukinoa kikosi hicho mara moja.
Shirikisho la soka nchini Saudia Arabia limetangaza maamuzi ya kocha Herve Renard kuachana na kikosi hicho na kutimkia timu ya taifa ya Ufaransa ya wanawake, Kocha huyo raia wa kimataifa wa Ufaransa alikua ana mkataba na Saudia Arabia mpaka mwaka 2027.
Kocha Herve Renard inaelezwa ametimkia timu ya taifa ya Ufaransa kwa ajili ya michuano ya Kombe la dunia ya wanawake ambayo itakwenda kufanyika nchini Australia mwishoni mwa mwaka huu, Na ndio inatajwa kama sababu kubwa ya kocha huyo kuachana na Saudia Arabia.
Kocha huyo atachukua mikoba ya Corrine Diacre ambaye ameachana na timu ya taifa ya wanawake ya Ufaransa, Huku kocha huyo wa zamani wa Morocco akichukua mikoba yake kwajili ya kukinoa kikosi hicho kwajili ya michuano ya kombe la dunia la wanawake nchini Australia.
Kocha Herve Renard ni kocha mwenye uzoefu mkubwa na timu za taifa kwani ameshawahi kuzifundisha timu kadhaa za taifa kabla ya Saudia Arabia na timu ya taifa ya wanawake ya Ufaransa, Kocha huyo ameshwahi kuifundisha Morocco na timu ya taifa ya Zambia akifanikiwa kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka 2012.