Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Herve Renard agoma kurejea Ivory Coast

Herve Renard (14).jpeg Herve Renard agoma kurejea Ivory Coast

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Herve Renard wa timu ya taifa ya wanawake ya Ufaransa amekataa kurudi kufundisha Ivory Coast.

Kwa sasa, Renard ni kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya Ufaransa na Ivory Coast ilikuwa imeliomba Shirikisho la Soka la Ufaransa "kumtoa kwa mkopo" kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 kuinoa Ivory Coast.

Ivory Coast ilimfuta kazi Jean Louis Gasset, aliyekuwa kocha msaidizi wa Ufaransa chini ya Laurent Blanc, na imemteua Emerse Fae kuwa mkufunzi wa muda japo walitumai kumrai Renard kuchukua nafasi ya kocha mkuu.

Renard ni mshindi mara mbili wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON, akiiongoza Zambia kushinda taji hilo mwaka 2012 walipoifunga Ivory Coast kwa mikwaju ya penalti na mnamo mwaka 2015 ambapo Ivory Coast iliifunga Ghana kwenye mechi ya fainali.

Renard amekuwa mjini Abidjan kutazama mechi za hatua ya makundi ya michuano hiyo kama mgeni wa serikali ya Ivory Coast.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live