Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro ameteua kamati maalum kwa ajili ya hamasa kwa timu za taifa zilizofuzu mashindano mbalimbali ya kimataifa.
Kamati hiyo inaundwa na Mwenyekiti, Theobald Sabi na makamu wake, Patric Kahemela pamoja na wajumbe wengine 17.
Rais wa Klabu ya Yanga, Hersi Said pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah maarufu Try Again ni miongoni mwa wajumbe hao.
Wengine ni: 1. Neema Msitha - Katibu
2. Beatrice Singano - Mjumbe
3. Michael Nchimbi - Mjumbe
4. Jemedari Said - Mjumbe,
5. Nick Reynolds (Bongo Zozo) - Mjumbe
6. Hamis Ali - Mjumbe
7. Christina Mosha (Seven) – Mjumbe
8. Paulo Makanza – Mjumbe
9. Mohamed Soloka - Mjumbe
10. Hassan Raza - Mjumbe
11. Lucas Mhavile (Joti) - Mjumbe
12. Oscar Oscar - Mjumbe
13. Prisca Kishamba - Mjumbe,
14. Burton Mwemba (Mwijaku) - Mjumbe,
15. Clayton Chipondo (Baba Levo) - Mjumbe.
Jukumu la kamati hiyo ni kuhamasisha wapenzi wa michezo kujitokeza kuzishangilia na kuziunga mkono timu za taifa pamoja na kuratibu hafla maalum ya harambee ya kuzichangia timu hizo. Harambee hiyo itafanyika Januari 10, 2024 jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Johari Rotana ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atamuwakilisha Rais, Samia Suluhu Hassan.