Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hersi: Sio Kisinda tu, kuna Yacouba, Tonombe

Hersi Pic Data Hersi: Sio Kisinda tu, kuna Yacouba, Tonombe

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

BAADA ya tetesi kuibuka kuwa winga wa Yanga, Tuisila Kisinda huenda akaachana na klabu hiyo na kutimkia Berkane FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco,  Mwanaspoti limeutafuta uongozi wa Yanga na kuzungumza.

Mjumbe wa kamati ya usajili ya Yanga, mhandisi Hersi Said ameweka wazi kuwa Yanga imepokea ofa ya Kisinda lakini bado hawajaafiki kumuuza na jambo hilo lipo katika meza yao likifanyiwa tathmini.

“Sio kwa Kisinda tu, tumepokea ofa za wachezaji wetu wengi wakiwemo Mukoko Tonombe na Yacouba Songne lakini hakuna hata mmoja ambaye tayari tumemruhusu kuondoka.

Ofa zote hizo zipo mezani kwetu na tunatumia umakini wa hali ya juu kuzitafakari na kuzitathimini na pale tutakapo pata jibu sahihi tutawajuza,” amesema Hersi.

Pia alipoulizwa kuhusu uwezekano wa Kisinda pamoja na nyota wengine kuondoka alijibu kuwa kama Yanga, mchezaji na timu atakayoenda wataafikiana vizuri kila kitu, biashara inaweza kufanyika.

“Yanga ni timu kubwa na suala la kuuza na kununua wachezaji linafanywa na timu kubwa duniani kote, kama Klabu, mchezaji na timu anayohitajika wakikaa meza moja na kuelewana basi biashara inaweza kufanyika,” amesema.

Kisinda alijiunga na Yanga msimu uliopita akitokea Maniema iliyokuwa imempekeka AS Vita (zote za Congo DR) kwa mkopo na kusaini mkataba wa miaka miwili, hivyo bado anamkataba wa mwaka mmoja na mabingwa hao wa kihistoria nchini Tanzania.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz