Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Herry Sasii kuamua nusu fainali Yanga vs Ihefu

Heri Sasii Herry Sasii kuamua nusu fainali Yanga vs Ihefu

Fri, 17 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwamuzi Herry Sasii kutoka Dar es Salaam amepewa dhamana ya kuchezesha mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la FA (CRDB) kati ya Ihefu Fc dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumapili May 19 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha .

Sasii atasaidiwa na Mohamed Mkono kutoka Tanga na Janeth Balama kutoka Iringa Mechi hiyo ya kusaka timu itakayocheza fainali dhidi ya mshindi wa mchezo kati ya Coastal Union dhidi ya Azam Fc, itapigwa saa 9 alasiri.

Yanga inasaka nafasi ya kucheza fainali ya tatu mfululizo na pengine kushinda taji hilo kwa msimu wa tatu mtawalia Kikosi cha Yanga kinajifua katika viwanja vya Bandari jijini Dar es salaam ambapo Wananchi wanatarajiwa kuelekea mkoani Arusha Ijumaa Tayari waapinzani wao Ihefu Fc wametua Arusha mapema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live