Straika wa zamani wa Yanga, Heritier Makambo amesema amejipa muda wa kujifua bila ya kuwa na timu kabla ya msimu ujao hajarejea nchini kuja kukiwasha, huku klabu mbili zilizopo Ligi Kuu zikitajwa kuanza mazungumzo naye.
“Nilikuwa na ofa nyingi baada ya kuachwa na Yanga lakini nikaomba kuachwa nipumzike dirisha kubwa ndio muda sahihi kwangu kuchagua ni timu gani ya kuitumikia kwa mafanikio.”
Hata hivyo, staa huyo aliyeifunga Yanga mabao manne anatajwa kuwindwa na Singida Big Stars na Namungo na alipoulizwa juu ya dili hizo, alisema kwa kifupi; “Ni suala la muda bado ni mchezaji lolote linaweza kutokea japo sijajua ni wapi nitacheza lakini nina mpango wa kurudi kiwanjani msimu ujao.”