Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Henry ataka kibarua Marekani

Thierry Henry K88iuwsme25d1f5tvxn0bin87 Thierry Henry

Sat, 18 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gwiji wa zamani wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Thiery Henry amesema yuko tayari kuchukua kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Marekani kama atapewa nafasi kama inavyosemekana.

Marekani wapo kwenye mkakati wa kutafuta kocha mpya wa kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya aliyekua kocha wa timu hiyo Gregg Berlahalter kumalizika mwishoni mwa mwaka jana, Taarifa zinaeleza kua gwiji Henry yupo kwenye orodha ya makocha ambao wanatajwa kupewa nafasi ya kua kocha wa timu ya taifa ya Marekani.

Thiery Henry kwasasa amekua na uzoefu baada ya kuu kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Ubelgiji vipindi viwili vya michuano ya kombe la dunia akianzia Urusi mwaka 2018, na Qatar mwaka 2018 hivo gwiji huyo yupo tayari kuchukua timu yeyote na kuiongoza kama kocha mkuu.

Marekani ambaye imepata nafasi ya kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2026 hivo inataka kujiandaa mapema na kutengeneza timu bora ambayo italeta ushindani kwenye michuano hiyo, Hivo wanahitaji kocha ambaye ataweza kuwafikisha kwenye nchi ya ahadi.

Gwiji Henry ambaye tayari ameshafundisha klabu moja na kua msaidizi wa timu ya taifa ya Ubelgiji kwa muda mrefu, Gwiji huyo ameonesha utayari wake pale alipoulizwa kuhusu kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Marekani ambayo inatafuta kocha kwasasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live