Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Henry aachia ngazi timu ya Taifa Ufaransa

Thiery Henry Thiery Henry.

Tue, 20 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Thierry Henry amejiuzulu nafasi yake ya kocha mkuu wa timu ya vijana ya Ufaransa chini ya miaka 21, baada ya kuiongoza kutwaa medali ya shaba kwenye mashindano ya Olimpiki 2024.

Henry (47) ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili aliifikisha timu hiyo fainali ya Mashindano ya Olimpiki na kufungwa na Hispania kwa mabao 5-3, lakini siku chache baada ya mashindano hayo ameachia ngazi.

Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal na Barcelona mkataba wake ulitarajiwa kumalizika mwakani baada ya mashindano ya Euro kwa vijana yanayotarajiwa kufanyika nchini Slovakia.

"Kutwaa medali kwenye mashindano ya Olimpiki ni jambo ambalo litabaki kwenye kumbukumbu ya muda mrefu sana kwenye maisha yangu,” alisema Henry kwenye taarifa yake.

"Ninapenda kulishukuru shirikisho, wachezaji pamoja na viongozi wengine wote wa ushirikiano ambao wamenipa. Lakini nimeamua kuachia ngazi nikiamini kuwa maamuzi yangu yana faida kubwa,” ilimalizia taarifa ya Henry.

Taarifa ya Shirikisho la Soka Ufaransa imesema kuwa ni taarifa ya kushtua kwa kuwa hawakuwa wanaitarajia.

Henry alifanikiwa kushinda michezo minne kati ya sita aliyofundisha akiwa kocha wa timu hiyo ya vijana kabla ya kwenda kwenye Olimpiki.

Mshambuliaji huyo alifanikiwa kucheza michezo 123 akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa na kufunga mabao 51.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live