Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Henry: Arsenal ilikuwa inatia kichechefu kuitazama

Henry France Thierry Henry

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Thierry Henry (46) amekiri kuwa alikuwa akitizama mechi za Arsenal kwa sababu tu ilibidi afanye hivyo.

Henry amedai kuwa ilikuwa ngumu kuitizama Arsenal wakati wa kipindi fulani cha Arsene Wenger na chini ya Unai Emery kwani timu hiyo ilikuwa ikihangaika.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia kutokea Ufaransa amesifia kikosi cha sasa huku akikumbukia mahangaiko ya timu hiyo kwa misimu kadhaa.

”Ilifika hatua nilikuwa naenda kwenye mechi kwavile tu ilibidi lakini si sababu nilikuwa nikitaka”

”Ni sababu tu nilikuwa shabiki wao, lakini sio kama nilivyotamani kuwaona wakicheza,lakini sasa naona mambo yanaenda vyema”

Bosi huyo wa timu ya Ufaransa ya vijana walio chini ya miaka 21 aliyasema hayo kabla ya ya mechi ambayo Arsenal iliishinda Manchester City kwa bao 1-0.

Henry alimsifia Mikel Arteta kwa kufanya kazi kubwa kuitoa timu hiyo mbali.

”Ninaheshimu sana alichokifanya Mikel, jinsi alivyoirudisha timu upya”.

Chini ya uongozi wa muda mrefu wa Wenger, Henry alikuwa mshambuliaji na mfungaji kiongozi wa Arsenal.

Alikuwa London Kaskazini kwa misimu nane , akanyanyua mataji mawili ya Ligi na Makombe matatu ya FA kabla ya kuondoka na kujiunga na Barcelona mwaka 2007.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live