Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Henock Inonga atimka Simba usiku

Inonga Hauzwi, Epukeni Matapeli   Ahmed Ally.jpeg Henock Inonga atimka Simba usiku

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki kisiki wa Klabu ya Simba raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Henock Inonga Bacca 'Varane' ameondoka nchini usiku wa kuamkia leo kuelekea nchini Ufaransa.

Kwa taarifa tulizonazo mchezaji huyu hatotumika kwenye michezo iliyobaki kwenye ligi kuu ya Tanzania pamoja na kwenda mapumziko mchezaji huyo anaenda Ufaransa kupata matibabu zaidi.

Inaelezwa kuwa, Inonga ameshataarifiwa na uongozi wa Simba kwa kile kinachoendelea baina yake na timu yake kuwa kwa sasa hatapata nafasi ya kucheza mpaka msimu huu utakapomalizika, huku msimamo wake wa kuondoka Simbaukiwa bado upo pale pale.

Aidha, taarifa zimekuwa zikidai kuwa tayari Inonga ameshasaini mkataba wa awali na AS Far Rabat Ya Morocco anayoinoa Nasreddine Nabi, na bada ya hapo amekuwa akikacha mechi ama kucheza chini ya kiwango kwa kile anachodai kuwa ni sababu ya majeraha.

Inonga ambaye alikuwa beki bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa kwanza alipotua Bongo, misimu miwili nyuma lakini ndani ya msimu huu, amecheza michezo 11 katika michezo 26 ambayo Simba wamecheza ambapo ameyeyusha dakika 769 pekee.

Inonga ambaye alikuwa beki Bora nchini Congo kabla ya kujiunga na Simba Agsti 15, 2021 kwa, mkataba wake unaisha Juni 30, 2025 hivyo bado ni mali ya Simba kama ataondoka simba watafanya biashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live