Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Henock Inonga arejea kikosini kuwavaa Singida FG leo

Henock Inonga Nje Siku 10 Henock Inonga arejea kikosini kuwavaa Singida FG leo

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema wanamshukuru Mungu kuona nyta wao wote waliokuwa majeruhi wanarejea kikosini.

Ahmed amesema, nyota wao Willy Onana ambaye alikuwa nje kwa muda kidogo, alirejea na wiki iliyopita alifanya balaa kwa kuwapa goli la ushindi dhidi ya Coastal Union pale Mkwakwani Stadium jijini Tanga lakini pia Henock Inonga naye amerejea.

"Inonga amerejea baada ya kupata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, ameanza mazoezi na wenzake na huwenda akawa sehemu ya mchezo wetu dhidi ya Singida FG," alisema Ahmed.

Simba anashuka dimbani leo katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar kukipiga na Singida FG ukiwa ni mchezo wao wa 18. Mpaka sasa, Simba ana alama 39 huku mpinzani wao wa jadi Yanga akiwa amecheza michezo 18 tayari akiwa na alama 49.

Endapo Simba akishinda leo na kuchukua alama tatu, atakuwa amepigwa gepu la alama 7 na Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live