Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson ametangaza kuondoka klabuni hapo baada ya kuwatumikia Majogoo hao kwa kipindi cha miaka 10 kupitia video fupi kwenye mitandao ya kijamii.
Ujumbe wa Henderson unaelezea safari yake klabu tangu alipotua klabuni hapo mnamo 2011 huku akiitaja hatua ya kufanywa nahodha wa klabu hiyo kama mojawapo ya ‘heshima kubwa maishani mwake’.
Aidha amebainisha kuwa kulikuwa na nyakati ngumu sana pia katika safari hiyo na pia amewashukuru mashabiki wa Wekundu hao kwa kumpokea na kumuuunga mkono kwenye nyakati nzuri na mbaya.
“Ni vigumu kuweka katika maneno miaka 12 iliyopita na ni vigumu hata kusema kwaheri. Siku zote nitakuwa Mwekundu. Mpaka siku nitakapokufa”
“Ahsante kwa kila kitu. You’ll never walk alone.” amesema.
Henderson (33) raia wa England ambaye ameichezea Liverpool mechi 492 akifunga magoli 39 na kutoa pasi (assists) 74 huku akitwaa mataji 8 yupo ukingoni kujiunga na klabu ya Al-Ettifaq FC ya Saudi Arabia inayonolewa na nahodha wa zamani wa Liverpool, Steven Gerald.