Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Henderson aponea tundu la Sindano kashfa ya Ubaguzi

Jordan Henderson Vs Gabriel Henderson aponea tundu la Sindano kashfa ya Ubaguzi

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson amekutwa hana hatia katika shutuma za ubaguzi ambazo alikua anakabiliwa nazo, baada ya uchunguzi kufanyika na shirikisho la mpira wa miguu England, FA limebaini mchezaji huyo hana hatia.

Wiki mbili zilizopita katika mchezo uliozikutanisha klabu za Liverpool na klabu ya Arsenal kulitokea mzozo baina ya Henderson na beki wa Arsenal Gabriel, Na ikitajwa kua mchezaji huyo alimbagua beki huyo mwenye asili ya rangi nyeusi.

Kutokana na tukio hilo shirikisho la mpira wa miguu nchini England, FA likafanya uchunguzi kubaini kama hizo shutuma ni za kweli kwa kiungo huyo wa kiingereza.

Baada ya uchunguzi kukamilika imebainika hakukua na ubaguzi wa aina yeyote uliooneshwa.

Kiungo Henderson amefanikiwa kutoka salama katika tuhuma hiyo ambayo shirikisho hilo imekua ikikemea kwa kiwango kikubwa na kusisitiza uungwana michezoni.

Baada ya hukumu hiyo kutoka wadau wengi wameonesha kutokuridhishwa na kuamini kua nahodha huyo alifanya vitendo vya kibaguzi lakini kama shirikisho limeamua kumtetea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live