Nahodha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya England, na Al Ettifaq Jordan Henderson amesema hataweza kuvaa mavazi yanayohamasisha mapenzi ya jinsia moja akiwa nchini Saudi Arabia.
Henderson amekuwa akishambuliwa kwa kitendo chake cha kujiunga na Ligi ya Saudi Arabia huku ikidaiwa kuwa wanakiuka sheria za kibinadamu.
Sasa akizungumza Henderson amesema;
"Kilichonipeleka Saudi Arabia ni changamoto mpya nilitaka kupata nafasi ya kucheza kila wiki na Sio pesa kama wengi mzaniavyo", Sikuwahi kuzungumza na Steven Gerrard kuhusu pesa"
"Naweza kuvaa Upinde wa Mvua lakini itakuwa sio vizuri kwa sababu nitakuwa sijaheshimu Dini na Utamaduni wa Saudia Arabia inabidi Tuheshimu"