Klabu ya Ajax imethibitisha kua kocha John Heitinga ataiongoza klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu huu baada ya kukaimu nafasi ya aliyekua kocha wa klabu hiyo kwenye mchezo mmoja.
Kocha John Heitinga alifanikiwa kuiongoza klabu ya Ajax katika mchezo mmoja wa ligi kuu ya Uholanzi na kufanikiwa kupata matokeo ya ushindi, Klabu ya Ajax imeamua kumkabidhi gwiji huyo wa zamani wa klabu hiyo timu aweze kuiongoza mpaka mwishoni mwa msimu huu.
Klabu ya Ajax iliweza kumfukuza kocha wake mkuu Alfred Schreuder ambaye alipitia kipindi kigumu katika klabu hiyo mpaka kufikia hatua ya kufukuzwa ndani ya timu, Kocha Schreuder alichukua mikoba ya Erik Ten Hag ndani ya timu hiyo aliyetimkia ndani ya Manchester United.
Kocha Alfred Schreuder mpaka anaondoka ndani ya Ajax aliiacha nafasi ya nne klabu hiyo ikiwa ni rekodi mbovu kwa klabu hiyo kwa miaka ya karibuni, Hivo klabu ya Ajax ikaamua kumuondoa kocha huyo na kumkabidhi timu kocha John Heitinga mpaka mwisho wa msimu.
John Heitinga anaweza kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuchukua kibarua cha kuinoa Ajax hata baada ya mwisho wa msimu huu, Hii itatokana na ubora ambao kocha huyo atauonesha ndani ya klabu ya Ajax akifanya vizuri gwiji basi atakua na nafasi kubwa ya kusalia klabuni hapo kwa muda mrefu.