Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hebu wasikie Klopp, Pep wanachosema

Best Coachesss Kocha wa City (kulia) na Liverpool wakiteta jambo

Wed, 13 Apr 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Pep Guardiola amesema Manchester City imeshindwa kuzima ndoto wa wapinzani wao Liverpool kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu na sasa kila kitu kipo wazi, yeyote anabeba.

Wakati Guardiola akisema hilo, kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alilinganisha vita ya Man City na Liverpool kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu na pambano la masumbwi la uzito wa juu, hivyo Man City imeshindwa kutumia fursa.

Man City ipo kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya pointi moja na kuna mechi saba zimebaki. Na Klopp baada ya kipute cha Etihad alisema: ìTunaweza kulielezea hili kama pambano la masumbwi la uzito wa juu. Ukishusha mikono kwa sekunde tu umepigwa. Hupaswi kutetereka, kwa sababu unaweza kupigwa na timu nyingine.

Mechi ya Etihad iliyotajwa kutoa taswira ya ubingwa, Kevin De Bruyne aliifungia Man City bao la kuongoza dakika ya tano tu, lakini Diogo Jota alisawazisha dakika nane baadaye. Gabriel Jesus aliwarudisha wenyeji kwenye uongozi tena, lakini Sadio Mane akachomoa na kufanya mechi hiyo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Guardiola naye alipoulizwa alisema: ìNdio hivyo, ni kama mchezo wa ngumi. Naona kabisa tumewaacha wakiwa na hai. Tulipoteza nafasi. Tulikuwa tunatazama pambano la ngumi.

Staa wa zamani wa Liverpool, Raheem Sterling aliifungia bao Man City, ambalo lingekuwa la ushindi, lakini VAR ilifuta bao hilo kwa madai ya mfungaji alikuwa ameotoea. Na Guardiola aliongeza: Kiwango chetu kimeshuka na hatuwezi kuwa mabingwa. Tushajua, unaposhuka tu, huwezi kushinda kitu.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz