Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hebu sikia hadithi ya Wenger

Arsene Wenger Predict Arsene Wenger

Sun, 5 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Arsene Wenger amefichua kwamba aligomea ofa nne za maana za kazi ikiwamo kwenda kuinoa Real Madrid na Barcelona wakati akiwa Arsenal.

Hilo liliwakosha mashabiki na kuamini kocha huyo kwa hicho alichokisema basi ukimchanja damu inayopita kwenye mishipa yake ni Arsenal.

Kocha huyo Mfaransa aliitumikia Arsenal kwa miaka 22 kuanzia 1996 hadi 2018. Na ndani ya muda huo, Wenger aliisaidia Arsenal kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu England na saba ya Kombe la FA.

Alichaguliwa mara zisizopungua tatu za kuwa kocha bora wa msimu na ni yeye pekee anayeshikilia rekodi ya kuiongoza timu kwenye Ligi Kuu England ikicheza msimu mzima bila ya kupoteza mechi hata moja.

Katika kipindi chake yupo Arsenal, Wenger alivutia timu nyingi ikiwamo vigogo wa La Liga Barcelona na Real Madrid, huku huko England, Manchester United iliripotiwa nayo kuhitaji huduma yake.

Wenger kwa sasa ni mmoja wa mabosi wakubwa Fifa, aliamua kumalizia ukocha wake kwenye kikosi cha Arsenal na tangu alipoondoka kwenye klabu hiyo ya Emirates hajachukua kazi yoyote ya ukocha.

Wenger alisema: “Real Madrid walinifuata mara mbili au tatu hivi. Na Barcelona walikuja mara moja.”

Chanzo: Mwanaspoti