Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

He! Trent aajiri mlinzi kisa demu

Trent Alexander Arnold He! Trent aajiri mlinzi kisa demu

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Staa wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold amekuwa akiandamwa kwa mwaka mzima na mwanamke anayemlazimisha awe mpenzi wake akituma meseji za mahaba na vitisho.

Kutokana na hilo, staa huyo wa Anfield amelazimika kuajiri mlinzi binafsi pamoja na mpelelezi binafsi kumfuatilia mwanamke huyo ambaye sasa amekuwa kero na kumtishia maisha.

Trent pia amelazimika kubadili namba ya simu, akifunga pia kamera za CCTV na kuweka alamu nyumbani kwake baada ya kupokea barua na vifurushi vingine vya zawadi kutoka kwa mwanamke huyo asiyejulikana.

Mwanamke huyo ameenda hadi nyumbani kwa Trent, mazoezini Liverpool na hata kwenye migahawa anayopendelea kwenda mkali huyo wa kimataifa wa England.

Kutokana na hilo, beki huyo, 26, ameshauriwa aachane kabisa na mambo ya mitandao ya kijamii. Familia yake pia imekuwa ikitumiwa meseji za vitisho.

Uongozi wa Liverpool unatambua hilo na unafanya kila wanaloweza kumsapoti mchezaji wao na chanzo cha habari kilieleza: “Hii kitu imekuwa hivi kwa mwaka sasa. Mwanamke huyo amekuwa akimsumbua Trent na familia yake, akituma meseji nyingi, akipiga simu muda wote na kutuma barua na vitu visivyoeleweka nyumbani kwake huko Cheshire.

“Amekuwa mtu wa wasiwasi muda wote, kitu ambacho amefanya ni kuacha hiyo kitu isiathiri mambo yake ya uwanjani.”

Chanzo: Mwanaspoti