Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

He! Kompany asakwa Bayern

Skysports Kompany Burnley 6114608 Vicent Kompany

Tue, 21 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Vincent Kompany ameshtua wengi kwa kuhusishwa na Bayern Munich baada ya timu aliyokuwa akiinoa, Burnley kushuka daraja Ligi Kuu England.

Kompany, 38, aliongoza Burnley kunasa taji la Championship na kuisaidia kupanda Ligi Kuu England mwaka jana, lakini walishindwa kupambana kwenye ligi hiyo na hivyo kushuka na kurudi Championship na itacheza msimu ujao.

Kwa mujibu wa gwiji wa masuala ya uhamisho, Fabrizio Romano, alisema Burnley kushuka daraja hili halizifanyi timu kuacha kufukuzia huduma ya gwiji huyo wa Manchester City akawe kocha kwao.

Miongoni mwa klabu zinazomtaka Kompany ni Bayern inayomtazama kama mtu inayoweza kumpa kazi endapo itaamua kuachana na Mjerumani, Thomas Tuchel.

Hiyo ina maana, Kompany anaweza kuhama kutoka soka la Championship hadi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Na Romano anafichua Brighton nao wanampigia hesabu pia wakati huu wakijaribu kusaka mrithi wa Roberto De Zerbi.

Bayern inapata shida kupata kocha mpya baada ya kushindwa kuwashawishi makocha wenye majina makubwa iliyokuwa ikiwataka. Ilimtaka Xabi Alonso, lakini Mhispaniola huyo aliamua kubaki Bayern Leverkusen.

Kocha wa Aston Villa, Unai Emery naye aliigomea miamba hiyo ya Allianz Arena, akisaini mkataba mpya huko Villa Park na msimu ujao watawaongoza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Bayern ilikataliwa pia na Ralf Rangnick na Julian Nagelsmann, huku kocha wa Benfica, Roger Schmidt, naye alihusishwa na miamba hiyo, lakini alikataa na kubaki zake Lisbon.

Kocha De Zerbi naye alihusishwa, lakini wakati akiondoka Brighton, bado haelezwi kwenda Allianz Arena.

Kinachoelezwa ni kocha huyo Mtaliano atakwenda mapumziko kwa muda na baada ya hapo ataamua.

Chanzo: Mwanaspoti