Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

He! Greenwood azua taharuki

Mason Greenwood First Debut He! Greenwood azua taharuki

Fri, 13 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyakazi wenye hasira wa Manchester United wamemjia juu Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Richard Arnold baada ya kutamka wazi kwamba walijisikia aibu kutokana na skendo ya Mason Greenwood.

Inafahamika kuwa wafanyakazi wa Old Trafford walionyesha kutoridhika na kauli ya mtendaji huyo wakati wa mkutano wa wafanyakazi wote.

Mkutano huo ulikuwa umeitishwa kutatua hofu juu ya kushughulikia kesi ya Greenwood licha ya kutolewa kwa mkopo Getafe.

Mshambuliaji huyo alifanyiwa uchunguzi wa ndani baada ya kukamatwa na tuhuma za ubakaji, na kutishia kuua kabla ya kumtoa kwa mkono lakini mabosi wameamua kujadili upya kupitia mkutano huo na wafanyakazi wote.

Aidha kesi za tuhuma za Greenwood ilitulipiliwa mbali na mahakama ya Greater Manchester Februari mwaka huu kabla ya kutolewa kwa mkopo katiak dirisha dogo la usajili Januari.

Kwa mujibu wa ripoti mkutano wa wafanyakazi wote ulifanyika Septemba 18 gazeti la The Athletic inaripoti kujadili ishu ya Greenwood.

Imeelezwa Wafanyakazi walialikwa kuwasilisha maswali bila kutaja majina yao kabla ya mkutano, na pia waliambiwa kutoa maoni kuhusu haki za wanawake ndani ya klabu hiyo.

Mfanyakazi mmoja wa kike inasemekana alishuhudia tabia zisizofaa kutoka kwa wafanyakazi wa kiume dhidi ya wafanyakazi wenzake wa kike.

Pia mtendaji huyo aliulizwa swali juu ya usajili wa winga wa Brazil Antony ambaye anatuhumiwa kumpiga mpenzi wake wa zamani.

Hata hivyo inasemekana alisisitiza kuwa klabu hiyo imetekeleza uangalizi wake, ikiwa ni pamoja na kuangalia rekodi za kisheria nchini Brazil.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live