Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

He! Eti Upamecano anaitwa Upamaguire

Maguire Harry Mm Mlinzi wa Man United, Harry Maguire

Sun, 23 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa soka wameachwa kwa kicheko cha kuvunja mbavu baada ya mtangazaji wa mechi ya Bayern Munich na Manchester City kumwita beki Dayot Upamecano jina la "Upamaguire” akiwa na maana ya kufanya makosa mengi uwanjani kama ambavyo amekuwa akifanya nahodha huyo wa Manchester United’.

Upamecano, 24, alikuwa akisifiwa kuwa mmoja wa mabeki bora kabisa duniani kabla ya Bayern hawajakutana na Man City kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Beki huyo Mfaransa alicheza hovyo kwelikweli kwenye mechi ya kwanza ambayo Man City ilishinda 3-0 uwanjani Etihad, kabla ya kurudia kucheza kwa kiwango cha hovyo kwenye mchezo wa marudiano wa sare ya 1-1 uliofanyika Allianz Arena usiku wa juzi Jumatano.

Upamecano alishindwa kabisa kumdhibiti Erling Haaland’. Alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhabu straika huyo ndani ya boksi, lakini aliokolewa na VAR ilipofuta kadi hiyo kwa madai Haaland alikuwa ameokoa.

Upamecano alifanya makosa mengine dhidi ya Haaland na safari hii, straika huyo wa kimataifa wa Norway aliweka mpira kwenye nyavu.

Mtangazaji wa mechi alishindwa kuvumilia kwa makosa hayo ya Upamecano na kumlinganisha na mtaalamu wa makosa mengi, beki wa Man United, Harry Maguire kwa kumwita Upamaguire.

Upamecano akiwa na mpira dakika tano za mwisho, mtangazaji huyo Mwarab alisema: “Upamaguire” kitu kilichowafanya mashabiki kuangua kicheko na kupendezwa na utani huo.

Shabiki wa kwanza aliandika: “Hebu subiri huyu mtangazaji amesema Upamaguire? Huu utani.”

Mwingine alisema: “Aaa hapana bro, Upamaguire!”

Shabiki wa tatu alisema: “Amemuita Upamaguire, huyu mtangazaji nampenda."

Upamecano huu ni msimu wake wa pili Bayern tangu aliposajiliwa kutoka RB Leipzig mwaka 2021 kwa ada ya Pauni 37 milioni. Amecheza mechi 77 tangu wakati huo na alishinda taji la Bundesliga msimu uliopita. Amechezea Ufaransa mara 14 tangu 2020.

Chanzo: Mwanaspoti