Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

He! Eti CR7 hamuwezi Hazard

Eden Hazard.jpeg Eden Hazard

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid, Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji, Eden Hazard amesema yeye ndiye bora kuliko Cristiano Ronaldo.

Hazard, 33, ambaye amestaafu soka Oktoba, 2023 alicheza kwa mafanikio makubwa akiwa na Chelsea aliyojiunga nayo akitokea Lille mwaka 2012.

Baada ya hapo alitua Madrid alipodumu kwa miaka minne iliyokuwa na maumivu makubwa kutokana na majeraha ya mara kwa mara aliyokuwa anakumbana nayo.

Alipoachana na Madrid alikuwa na nafasi kutua Saudi Arabia na baadhi ya timu barani Ulaya lakini alichagua kustaafu na kutulia.

Alipofanya mahojiano na gazeti la Ufaransa L’Equipe, Hazard alisema yeye anaweza kuwa bora zaidi ya Ronaldo.

“Ukitazama kwa kiwango cha mchezaji mmoja mmoja Messi ni bora, nilikuwa napenda kutazama wachezaji wa Barcelona ni ngumu sana kuuchukua mpira ukiwa miguuni mwake, Cristiano ni mchezaji mkubwa kuliko mimi lakini kwenye sekta ya nani ana kipaji sioni kama ananifikia, labda Neymar. Baada ya hapo sidhani kama Ronaldo ni bora kuliko mimi “

Messi na Ronaldo wamecheza mechi nyingi, wamefunga mara nyingi na kutoa asisti mara nyingi zaidi ya vile ambavyo Hazard amefanya alipokuwa anacheza.

Ronaldo, ambaye leo ametimiza umri wa miaka 39, amefunga mabao 867 kwenye mechi1, 198 katika maisha ya soka pia ametoa asisti 282.

Messi yeye amefunga mabao 821 katika mechi 1,033 tangu aanze kucheza soka la kulipwa, pia ameshinda tuzo nane za Ballons d’Or, huku Ronaldo akiwa na tano.

Messi ameshinda mataji tisa ya Ligi ya Mabingwa sawa na Ronaldo ambaye aliisaidia Ureno kuchukua taji la mashindano ya Euro mwaka 2016 wakati Messi akiisaidia Argentina kuchukua Kombe la Dunia kule Qatar mwaka 2022.

Hazard, yeye amefunga mabao 200 na kutoa asisti 193 kwenye mechi 748.

Chanzo: Mwanaspoti