Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

He! Bingwa Carabao kuvuna Sh322 milioni tu

Liver Carabao He! Bingwa Carabao kuvuna Sh322 milioni tu

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Juna Jumapili Februari 25 katika dimba la Wembley mida ya saa 12:00 jioni, Chelsea na Liverpool zilikutana katika mchezo wa fainali ya Kombe la Carabao ambapo mshindi atapokea zawadi ya Pauni 100,000 ambazo ni sawa na Sh322 milioni za Kitanzania.

Mechi hiyo iliyomalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Chelsea, taarifa zinaonesha timu iliyopoteza itapata Pauni dola 50,000 ambazo ni sawa na Sh161 milioni za Kibongo.

Kwa upande wa timu zilizoishia hatua ya nusu fainali, Fulham na Middlesbrough zenyewe zitapata Pauni 25,000 ambazo ni Sh80 milioni kwa pesa ya Tanzania.

Pesa hii ni kidogo sana ukilinganisha na kiasi ambacho anakipata bingwa wa Ligi Kuu England ambacho kinafikia Pauni 150 milioni huku bingwa wa Kombe la FA hutia kibindoni Pauni 4 milioni.

Chanzo: Mwanaspoti