Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

He! Baada ya Feisal, Azam FC wageukia kwa Simba SC

EC2D5DB9 41B6 49F7 AC55 366BF253AE9A.jpeg Beki wa Simba, Henock Inonga Baka

Mon, 26 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Saa chache baada ya kuwavuruga mashabiki na wanachama wa Yanga kwa kumng’oa kibabe kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’, klabu ya Azam FC imedaiwa sasa imeamua kuwageukia Simba, ikipiga hesabu ya kumchomoa mmoja ya nyota wa kikosi cha timu hiyo inayoshika nafasi ya pili ya Ligi Kuu Bara.

Azam inayoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu, inadaiwa kumalizana na Fei Toto baada ya kiungo huyo kuvunja mkataba kwa kuilipa Yanga Sh112 milioni, zikiwamo Sh12 milioni za mishahara ya miezi mitatu kulingana na vipengele vya mkataba baina yao ili apate nafasi kuondoka.

Lakini, wakati wadau wa soka wakiendelea kujadili dili la Fei na wengine kudhani labda Azam imeshamaliza kasi, matajiri hao wa Bongo wameliamsha tena kwani kwa sasa ikianza mipango ya kumng’oa beki kisiki wa Simba, Henock Inonga Baka.

Beki huyo wa kati wa Simba kutoka DR Congo ameongeza mkataba utakaomuweka Msimbazi hadi 2025 na Azam imefanya mazungumzo na menejimenti yake tayari kumvuta Chamazi kwenda kushirikiana na mabeki wengine wa kati wa timu hiyo.

Habari za kuamini kutoka ndani ya Azam zinasema kuwa, mabosi wa timu hiyo wameanza mchakato ili kwenda kuimarisha ukuta wa timu hiyo na mazungumzo kupitia menejimenti ya Mkongoman huyo imefikia pazuri na muda wowote beki huyo atasainishwa mkataba ili aungane na kina Idris Mbombo.

Mmoja ya rafiki wa karibu wa beki huyo, alidokeza kuwa, pande mbili zipo kwenye mazungumzo mazuri kupitia wakala wa mchezaji, ili atue Chamazi na kulikuwa na ishu ya masilahi ndio hawajamalizana nao.

“Kila kitu kinaonekana kinaenda sawa, tayari mazungumzo yameanza na kilichobaki ni pande mbili kuafikiana kabla ya mabosi wa Azam kuwafuata wenzao wa Simba ili kukubaliana kwani bado ana mkataba na Azam imeonyesha haitanii kwani ipo tayari kutoa mkwanja wowote,” kilisema chanzo hicho za kuaminika.

Kama Inonga atatua Azam ataungana na Daniel Amoah, Malickou Ndoye pamoja na Abdallah Kheri ‘Sebo’ wanaosimama beki ya kati ya timu hiyo ambayo hadi sasa katika ligi imeruhusu jumla ya mabao 16 katika mechi 17 ikiwa ni wastani wa kila mechi moja imefungwa bao moja.

Inonga alisajiliwa misimu miwili iliyopita na amekuwa mmoja ya mhimili imara wa timu hiyo ambapo kwa misimu yote akishirikiana na Joash Onyango na wakati mwingine ilikuwa Pascal Wawa na Kennedy Juma na kuifanya Simba iwe timu ngumu kufungika. Kwa sasa Simba imeruhusu mabao nane kama iliyofungwa Yanga katika mechi 17 za msimu huu. Msimu uliopita Simba iliruhusu mabao 14 katia mechi 30, huku Azam ikifungwa 28 kwa idadi ya mechi kama hizo.

Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin ‘Popat’ alipoulizwa jana juu ya dili hilo, aliiishia kucheka na kusema subiri muda utaongea kwani kwa sasa akili zao zipo kwenye mechi ya leo dhidi ya Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live