Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hazard kuwapa tena real Madrid hasara

Eden Hazard 1140x640 Eden Hazard

Fri, 17 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kustaafu, Chelsea inatarajiwa kukunja Pauni 5 milioni kutoka Real Madrid ikiwa ni moja kati ya vipengele vilivyokuwepo katika makubaliano ya kumuuza aliyekuwa staa wao, Eden Hazard mwaka 2019.

Hazard ambaye amestaafu Oktoba mwaka jana, alijiunga na Madrid kwa ada ya uhamisho ya Pauni 88 milioni mwaka 2019 na kusaini mkataba wa miaka mitano ambao ulikuwa unamalizika mwisho wa msimu huu.

Lakini mbali ya Pauni 88 milioni, pia dili hilo lilikuwa na pesa za nyongeza ambazo Chelsea wanazipata kutokana na kiwango cha mchezaji na timu kwa jumla wakati wa mkataba huo.

Kwa mujibu wa taarifa, hadi sasa Chelsea imepata kiasi kisichopungua Pauni 130 milioni na kijumla inaweza kupata hadi Pauni 150 milioni.

Licha ya Hazard kustaafu miezi saba iliyopita, bonasi bado zinatakiwa kulipwa hadi mwisho wa msimu huu na mkataba utamalizika.

Hivi sasa Chelsea inatakiwa kulipwa Pauni 5 milioni baada ya Madrid kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mujibu wa Telegraph.

Usajili wa Hazard kwenda Madrid unaonekana kuwa moja kati ya madili yaliyofeli sana katika kipindi cha hivi karibuni kwa sababu mchezaji mwenyewe hakuonyesha kiwango kilichotarajiwa.

Ndani ya misimu minne, Hazard alicheza mechi 76 tu za michuano yote, akafunga mabao saba na kutoa asisti tisa.

Hiyo ilikuwa tofauti kabisa na kile alichoonyesha ndani ya misimu sana aliyodumu na Chelsea ambapo alishinda mataji mawili ya Europa League, FA Cup, EFL na Ligi Kuu England mara mbili.

Chanzo: Mwanaspoti