Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hazard kufanyiwa Upasuaji, Madrid wathibitisha

Eden Hazard.jpeg Winga wa Real Madrid, Eden Hazard

Sat, 26 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaj nyota ya Real Madrid Eden Hazard anatarajia kufanyiwa upasuaki mwingine wa kuondoa “osteosynthesis plate” kwenye mguu wake wa kulia ambayo yanatarajia kumuweka nje kwa mwezi moja.

Eden Hazard ambaye alisajiriwa kwa ada ya uhamisho wa £98million akitokea Chelsea mwaka 2019 akienda Madrid, amefanilkiwa kucheza michezo 65 tu, huku akishindwa kupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha Los Blancos kutokana na kupata majeruhi ya mara kwa mara.

Majeruhi haya yaatamuweka nje ya kikosi cha Real Madrid ambacho kitacheza dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya mwezi ujao.

Eden Hazard atafanyiwa upasuaji wa kuondoa ‘plate’ ambayo aliwekewa kwenye mguu wake wa kulia baada kuvunjika March 2020.

“Kwa siku kadhaa zijazo, mchezaji wetu Eden Hazard, atafanyiwa upasuaji wa kuondoa ‘osteosynthesis plate’ kwenye mguu wake wa kulia ndani ya ‘fibula”, waraka wa klabu ulisema.

Hazard amecheza michezo 22 tu msimu huu huku akianza kwenye michezo 8 ya La Liga wakati akifunga goli moja na kusaidi kupatikana mawili, pia haja fanikiwa kucheza tena tangu alipoingia kwenye mchezo dhidi ya Alaves February 19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live