Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hazard atupia na kutoa assist

Hazardss Eden Hazard.

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa zamani wa Chelsea na Real Madrid, Eden Hazard ambaye alitangaza kustaafu soka majuzi ameonesha kuwa bado ana tuvitu-vitu miguuni baada ya kung'ara kwa kufunga bao na kumpasia babake na Mbappé, katika mchezo wa kirafiki wa hisani.

Hazard ambaye aliwakilisha Varietes CF dhidi ya Team Calais alitoa pasi maridadi kwa Wilfried Mbappé baba wa nyota wa PSG Kylian ambaye aliifungia timu hiyo bao la 6 katika mchezo huo.

Timu ya Hazard aliungana na nyota wengine wa zamani kama Ludovic Giuly, gwiji wa Arsenal Robert Pires katika safu ya ushambuliaji, huku Didier Deschamps, Claude Puel na Yohan Cabaye wakishikilia kiungo.

Kwenye nafasi ya ulinzi kulikuwa na Christian Karembeu, beki wa zamani wa Bayern, Daniel Van Buyten, Laurent Blanc and Mathieu Debuchy huku golini akisimama nyanda wa zamani wa Arsenal na Ujerumani, Jens Lehmann.

Mechi hiyo ya hisani ilichangisha takriban pauni 12,900 ambazo zitatumika kuwasaidia watoto na vijana katika hospitali ya Pieces Jaunes.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live