Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hazard: Chelsea mpeni timu Fabregas

Eden X Fabregas Hazard: Chelsea mpeni timu Fabregas

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa, Eden Hazard amewataka mabosi wa Chelsea wasihangaike sana juu ya kumpata kocha mpya, bali wafanye haraka kwenda kumpa kazi hiyo, Cesc Fabregas.

Hazard, ambaye ni staa wa zamani wa Chelsea anaamini mchezaji mwenzake huyo wa zamani wa Stamford Bridge, Fabregas anafaa kabisa kukabidhiwa mikoba ya ukocha kwenye kikosi hicho.

Cesc ameisaidia Como kupanda daraja huko Italia na kucheza Serie A akiwa mmoja kwenye benchi la ufundi la timu hiyo.

Wakati Chelsea kwa sasa ikihangaika kutafuta kocha mpya, Hazard aliambia talkSPORT: “Pengine Roberto de Zerbi. Nina rafiki yangu pia yupo Como. Anafaa kuwa kocha.”

Katika ishu ya Mauricio Pochettino kuondoka, Hazard alisema: “Ilikuwa huzuni kubwa kwa kusema ukweli. Nadhani amefanya kazi kubwa. Nafahamu watu wanataka Chelsea iwe kwenye Top Four, lakini huu ni msimu wa mpito.

“Yeye ni kocha mzuri na namtakia kila lenye heri. Acha tusubiri tuone ni kitu gani kitaendelea.”

Chelsea ilimaliza nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu wa 2023-24, lakini imepokwa tiketi ya kucheza Europa League na badala yake itacheza kwenye Europa Conference League baada ya Manchester United kushinda ubingwa wa Kombe la FA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live