Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haya ndio usiyoyajua kuhusu Tuzo ya Ballon D'or

BDR Power Ranking Haya ndio usiyoyajua kuhusu Tuzo ya Ballon D'or

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati mshindi wa Tuzo ya Ballon D'or ikitarajiwa kutolewa leo Oktoba 30 pale katika Jiji la Paris nchini Ufaransa.

Haya ndio mambo makuu ya msingi unayopaswa kuyafahamu kuelekea siku hii muhimu.

1. Jina la mshindi wa tuzo ya Ballon D’Or huchorwa siku chache kabla ya sherehe na zoezi hilo hufanywa kwa usiri wa hali ya juu bila watu kujua

2. Tuzo hii inayotolewa sasa ilianzishwa mwaka 1983 na ilichukuliwa kwa mara ya kwanza na Michel Platini.

3 .Cristiano Ronaldo ameteuliwa kuwania tuzo hii [Ballon d'Or ] mara kumi na nane, na ni mshindi kwa mara tano tu .

4. George Weah alikuwa mchezaji wa kwanza mwenye asili ya Afrika kushinda tuzo hiyo yenye heshima kubwa Duniani .

5 . Lev Yashin ndiye golikipa pekee aliyeshinda tuzo hiyo tangu kuanzishwa kwake

6. Kila Ballon D'or ni ya kipekee na hata muonekano ambao hutumika kama msingi wa tuzo hauna umbo sawa kabisa na tuzo zilizotangulia ,hiyo ina inafanya hata uzito hutofautiana ingawa uzito unakadiliwa kufikia kilo 12 .

Fact nyingine ambayo sio rasmi sana ila itakusaidia kupunguza presha usiku wa leo ni kwamba mara zote huwa ni ngumu sana mchezaji kushiriki kwa mara ya kwanza na kushinda tuzo hii !

Kwa facts hizo kura yako unaiweka kwa nani yakiwa yamebaki masaa machache kabla ya tuzo kutolewa ____?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live