Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haya ndio matukio muhimu yaliyojitokeza kipigo cha Mazembe kwa Mkapa

Mashabiki Wa Yanga Mkapa Mashabiki waliojitokeza kuishangilia Yanga Jumapili iliyopita

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga iliichapa TP Mazembe mabao 3-1 katika kampeni ya mechi za hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Huo ni ushindi wa kwanza kwa Yanga mbele ya Mazembe tangu timu hizo zilipokutana, Wakongomani hao wakishinda mara mbili na kutoa sare moja.

Ndani ya mchezo huo kuna matukio ambayo yalibeba upekee ambayo hayakuonekana Moja kwa moja katika furaha ya ushindi wa Yanga.

WAFUNGAJI WALIJIPANGA

Bao la kwanza lilifungwa kwa kichwa na Kennedy Musonda ambaye anavaa jezi namba 25 mgongoni.

Mfungaji wa bao la pili la Yanga alikuwa ni Mudathir Yahya lakini kumbuka kiungo huyo anavaa jezi namba 27.

Bao la tatu lilifungwa na winga Twisila Kisinda aliyeingia kipindi cha pili kwa shuti kali jamaa anavaa jezi namba 29 na kufanya mabao hayo kufungwa na wachezaji wenye jezi zinazopishana kwa namba mbili tu.

AS VITA YAICHAPA MAZEMBE DAR

Inawezekana ukawa ni ushindi wa Yanga mbele ya TP Mazembe, lakini hata kule DR Congo kuna klabu imeshangilia ushindi huo na sasa nao wanataka jezi za Yanga.

Yanga ina wachezaji sita wa Kongo ambapo kati ya hao watano walianza kikosi cha kwanza huku mmoja akianzia benchi na wote walipiga kazi ya kibabe uwanjani.

Anza na Djuma Shaban kama beki wa kulia, lakini adhabu hiyo ilitokana na ubora wa winga Jesus Moloko ambaye ndiye aliyeangushwa na kuzalisha shambulizi hilo. Beki wa kushoto, Lomalisa Mutambala alikuwa katika kiwango bora.

Yannick Bangala alikuwa katikati ya uwanja kama kiungo aliyewavuruga Mazembe na kulazimisha kufanya mabadiliko ya haraka dakika 30 za kwanza.

Kule mbele mtu hatari alikuwa Fiston Mayele aliwakimbiza mabeki wa Mazembe alivyotaka alikosa bahati tu ya kufunga lakini akapika bao la mwisho lililomaliza mechi.

NABI NA PICHA

Sijui ni lini mara ya mwisho Nabi kupiga picha na wachezaji wake kabla ya mechi kuanza hasa ya mashindano kwenye mechi ya Mazembe akaitaka hiyo picha kumbuka huyu ni kati ya makocha wasiokuwa na akaunti yoyote ya mitandao ya kijamii lakini upekee zaidi alionekana kwa mara ya kwanza uwanjani wakati timu yake inapasha misuli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live