Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haya hapa Majukumu ya Kaze Yanga

KAZE.png Kocha msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze

Thu, 30 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema moja ya kitu ambacho anashukuru ni urejeo wa Cedric Kaze kwenye timu hiyo kwa kuwa amekuja kufanya kazi yake iwe nyepesi.

Nabi aliyataja majukumu ya Kaze kwenye timu hiyo kuwa ni kumsaidia kuwasilisha programu kwa wachezaji kwa kuwa yeye ni mjuzi wa mambo na faida kubwa aliyonayo ni uwezo wa kuzungumza lugha zote ambazo wachezaji wa Yanga wanazungumza ambazo ni Kingereza, Kifaransa na Kiswahili.

Akizungumza na Spoti Xtra, Nabi amesema kabla ya ujio wa Kaze kwa kipindi ambacho alikuwa anafanya kazi peke yake alikuwa anapitia wakati mgumu kwa sababu alikuwa anafanya kazi nyingi kwa wakati mmoja jambo ambalo lilifanya awe anachoka sana.

“Najikuta mwenye bahati sana msimu huu kutokana na urejeo wa Kaze kwenye timu, Kaze ni mjuzi wa kazi zetu na aliwahi kupita hapa na anaifahamu timu na wachezaji vizuri sana.

“Atakuwa msaada mkubwa sana kwenye timu yetu kwa sababu anajua kuzungumza lugha zote ambazo wachezaji wa Yanga wanazungumza jambo ambalo awali lilikuwa linanipa ugumu na kupelekea kufanya kazi kubwa kila siku,” amesema Nabi.

Katika hatua nyingine, Nabi ameomba siku 30 kwa ajili ya kuimarisha zaidi kikosi chake kiwe na makali zaidi kwa msimu huu.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amesema “Hatukuwa na muda wa kujiandaa zaidi kama wenzetu ila kwa sasa Kocha Nabi ameomba siku 30 zaidi za kuiandaa timu bora zaidi ya ile iliyocheza na Simba".

“Malengo yetu sio tu kumzuia Simba kuchukua ubingwa, bali tunataka kumzidi kwa pointi ili tuchukue ubingwa wa ligi kuu kwa msimu ujao.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live