Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawakuvaa jezi za Yanga, walivaa Bendera ya Tanzania

Yanga Msgdd Hawakuvaa jezi za Yanga, walivaa Bendera ya Tanzania

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni katikati ya Wanadamu ambao wana imani kubwa yakuwa elimu ni maalumu kuanzia umri wa miaka 8 hadi 30, na baada ya hapo ni muda wa kuteseka na changamoto za maisha.

Ni imani kali zaidi ya YOU WILL NEVER WALK ALONE pale Anfield,lakini katikati ya imani hii kuna shujaa wa kike Hayati PRISCILLA SITIENEI ambaye aliamua kurudi Darasani akiwa na umri wa miaka 94, unajua kwanini? Sababu alitaka atuoneshe yakuwa Elimu haina mwisho, that's reality, USIGEUKE NYUMA MUSA NISHAPASUA BAHARI UTAFUNIKWA NA MAJI.

Katikati ya uwanja wa kivita umbao unaitwa OMAR STADIUM kulikuwa kuna Wanaume 11 ambao walitumwa na Taifa.

Ni usiku ambao ni wa kumbukumbu kwa Wanaume hao 11, ulikuwa ni usiku ambao majukwaa yote ya pale OMAR STADIUM yaliduwaa na wapambanaji kutokea Kusini mwa Jangwa la Sahara, ni vijana ambao wengi wao walitokea maisha ya kimaskini na waliamini mpira utawapa dili .

OMAR STADIUM hakukuwa tena kiwanja cha mpira bali ulikuwa ni uwanja wa vita ambao uliacha historia kubwa , historia ya masela fulani hivi ambao waliotoka kuwa Underdogs hadi kuwa timu inayotisha Afrika , kutoka kuitwa timu yenye viongozi wasela hadi kuwa Wasomi.

Ni hadithi zenye kusisimua ambazo mashabiki wa Usm Alger waliziogopa hadi wakaanza kupiga baruti ili muda ukimbie maana hali ilikuwa taabani , hapakuwa tena OMAR STADIUM bali palikuwa ni BENJAMIN MKAPA pro max.

Wala hawakuvaa jezi za YANGA bali walivaa Bendera ya Taifa la JK WAKWANZA, walipewa roho ngumu ya CHE GUEVARA, Busara za Nelson Mandela maana Omar Stadium haikuwepo fujo kutoka kwao, wenyewe masela waliwaza ushindi.

Kwenye Makashablasha ya kumbukumbu pale Ikulu kwa MAMA SAMIA, wale Viongozi wasela wameandikwa waliingia na medali, ile timu iliyowafunga wale mliosema ni wadhaifu tayari Kumbukumbu zao zipo Ikulu. KUMBUKUMBU HAZIFUTIKI na hiyo ndio TBT yangu leo hii .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: