Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawabebi Ubingwa, wasahau

Yanga Ubingwa No Mipango ya Yanga msimu huu haitakwama kubeba Ubingwa

Mon, 21 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga ipo kambini ikiendelea na maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya Mtibwa Sugar, huku kocha Nasreddine Nabi akisisitiza hataki kusikia chochote msimu huu, zaidi ya kubeba ndoo, lakini akiipika safu yake ya ushambuliaji.

Katika tizi la juzi kambini Avic, Kigambini kocha Nabi alikomaa na washambuliaji wake ili kuongeza umakini wa kufunga na habari njema ni kwamba staa wao Fiston Mayele jamaa anauwasha moto hadi mazoezini.

Mayele katika mazoezi hayo ya alikuwa mwiba akifunga mabao matano tofauti, lakini Nabi alipomaliza mazoezi hayo aliwabakisha washambuliaji wake wengine wawili, Yusuf Athuman na Heritier Makambo.

Kubaki kwao hapo pia Nabi akawabakiza mabeki wawili wa kati Ibrahim Bacca na beki mmoja wa kutoka timu ya vijana kisha kila mmoja kumtaka kupambana kufunga.

Washambuliaji hao walikuwa wakipewa mipira tofauti na viungo wa pembeni Dickson Ambundo na Denis Nkane kisha kutaka Makambo na Yusuf kufunga, huku langoni kukiwa na makipa wawili tofauti kwa kila goli Eric Johora na chipukiz Geofrey Magaigwa.

Mazoezi hayo yalikuwa maalum kwa washambuliaji hao, Nabi akitaka kuona wanakuwa bora katika kufunga na Yusuf alifanya vizuri kuliko Makambo. Advertisement

Yusuf anayepambana kurejea katika ubora akitokea majeruhi alifunga mara tatu, huku Makambo akifunga mara moja kabla ya kuumia kwa kugongana na Bacca.

MATIZI YA FEI TOTO

Naye kiungo Feisal Salum alikuwa na moto akionyesha ubora wa kufunga mazoezi ya pamoja na wenzake akifunga mara nne.

Kiungo huyo alipigishwa tizi la maana na kuonyesha kama wapinzani wa Yanga wakikaa kizembe wataumia kwa jinsi alivyoonyesha kuiva zaidi hasa kwa pasi mbali na kufunga.

Hadi sasa katika Ligi Kuu, Fei Toto amefunga mabao manne akilingana na Saido Ntibazonkiza wakiwa nyuma ya kinara Fiston Mayele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live