Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawa wote wamekuwa wapenzi watazamaji

African Football Afl Hawa wote wamekuwa wapenzi watazamaji

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hizi ni timu ambazo zilishiriki michuano mipya ya African Football League (AFL) na zikashuhudia Mamelodi Sundowns wakiandika historia ya kutwaa Ubingwa wa AFL.

Mamelodi Sundowns (Bingwa)

-Simba Sc

-Al Ahly SC

-Enyimba Fc

-TP Mazembe

-Petro De Luanda

-Esperance de Tunis

-Wydad Athletic Club

Pesa ambazo kila timu zimepata kwa kile walichokionyesha ndani ya michuano hii Simba Sc, Petro De Luanda, TP Mazembe na Enyimba Fc wote wamefanikiwa kuondoka na kitita cha Bilioni 2.5 za kitanzania.

Al Ahly na Esperance De Tunis, wamefanikiwa kupata bilioni 2.5 za kushiriki na bilioni 4.2 za kufika hatua ya nusu fainali ya michuano ya African Football League.

Wydad Athletic Club wamepata bilioni 2.5 za kushiriki michuano hiyo, bilioni 4.2 za kutinga hatua ya nusu fainali ya African Football League na Bilioni 7.5 za kuwa washindi wa pili wa michuano hiyo.

Mamelodi Sundowns ambaye ni Mabingwa wa African Football League wepata bilioni 2.5 za kushiriki + bilioni 4.2 za kutinga hatua ya nusu fainali + bilioni 9.9 za kuwa bingwa wa michuano hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live