Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawa watacheza wapi msimu wa 2024/25?

Salah Sancho Greenwood Adsfc Hawa watacheza wapi msimu wa 2024/25?

Thu, 27 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dirisha la usajili la majira ya kiangazi limezidi kupamba moto huku wachezaji kadhaa tayari imeshajulikana watacheza wapi msimu ujao baada ya tetesi za muda mrefu.

Hata hivyo, kuna wengine bado wanaacha maswali juu ya jezi gani watavaa kwani hadi sasa hakuna uelekeo wa timu watakazojiunga nazo huku timu nyingi zikionekana kuhitaji huduma zao.

Mbali ya wachezaji pia kuna makocha walioingia katika tetesi za kuhusishwa na timu mbalimbali na hadi sasa bado hawajasaini kufundisha timu yoyote.

Hapa kuna wachezaji na makocha ambao maswali ya wapi watatua dirisha hili yanasubiriwa kwa hamu yanawahusu.

5. Mason Greenwood

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, Man United haina mpango wa kumrudisha tena katika kikosi chao na hiyo imezipa nguvu zaidi timu zinazomhitaji ambazo ni Barcelona, Atletico Madrid, Lazio na Juventus kuwa zinaweza kumpata.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna timu iliyoonekana kuwa na asilimia zaidi ya 70 za kumpata kwa sababu hakuna mazungumzo ya kina yaliyofanywa kwa mujibu ripoti mbalimbali.

Hili nalo limebakiwa kuwa swali ambalo linasubiriwa kwa hamu kujibiwa dirisha hili ingawa pia kuna tetesi zinazomhusisha na timu za Saudia.

4. Mohamed Salah

Katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana, Al Ittihad ya Saudi Arabia ilimwekea mezani mshahara wa zaidi ya Pauni 100 milioni kwa mwaka ili akubali kujiunga nao, akakataa.

Baada ya kukataa ofa hiyo kubwa ikaeleza anataka kusubiri hadi mwisho wa msimu uliomalizika ndio aondoke.

Kwa miezi kadhaa taarifa mbalimbali kutoka England zinadai staa huyo ameshawasilisha hadi barua ya kuomba kuondoka kwa sababu bado ana mkataba unaomalizika mwakani.

Lakini hadi sasa hakuna taarifa yoyote juu ya nini kinaendelea kwa staa huyu, ikiwa ataondoka kutua Saudi Arabia au atabaki.

3. Roberto De Zerbi

Baada ya kuondoka Brighton, taarifa zilidai anaweza kutua Chelsea, Manchester United au Barcelona ambazo ndio zilikuwa zinatafuta makocha kwa wakati huo.

Lakini timu hizi zote zimeshaajiri makocha wengine na bado De Zerbi hajapata timu huku tetesi zikieleza yupo katika hatua za mwisho kusaini mkataba wa kuinoa Marseille ya Ufaransa ingawa nako hakujawa na uhakika wa asilimia mia.

Swali la De Zerbi ataenda wapi limezidi kuchanganya mashabiki wengi.

2. Victor Osimhen

Napoli ipo tayari kumwachia fundi huyu wa kimataifa wa Nigeria ikiwa timu inayomhitaji itatoa Euro 100 milioni ambayo imewekwa katika kipengele cha kuuvunja mkataba wake.

Timu kibao zinamhitaji ikiwemo PSG, Chelsea, Arsenal na matajiri wa Saudi Arabia lakini hadi sasa haijajulikana atatua wapi.

Mkataba wake unamalizika mwaka 2026, anaweza akajiunga na timu yoyote kati ya hizo tajwa hapo juu na usajili wake umeendelea kuwa swali ambalo mashabiki wengi wanasubiri kwa hamu lijibiwe.

1. Jadon Sancho

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag anadaiwa yupo tayari kumruhusu staa huyu arudi katika kikosi cha Manchester United lakini kwa sharti la kuomba msamaha.

Hadi sasa haijajulikana ni wapi atatimkia ingawa kuna timu kibao ikiwa pamoja na Barcelona, Juventus na Borussia Dortmund yenyewe ambayo inahitaji kumrudisha tena kwa mkopo kwa msimu ujao au kumnunua mazima.

Sancho mwenyewe anaripotiwa kuwa anahitaji kuondoka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live