Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawa ndo hatari pale Yanga - Kocha KMC

Nzengeli Muda Hawa ndo hatari pale Yanga - Kocha KMC

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Mkuu wa KMC, Abdihamid Moalin amewataja wachezaji wa Yanga, Maxi Mpia Nzengeli na Mudathir Yahya Abbas kuwa ndiyo wachezaji tishio ndani ya kikosi hicho, hivyo amejiandaa kuhakikisha anawadhibiti ili wasiwe na madhara kwenye lango la timu yake.

Moalin amesema hayo jana Jumanne, wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wa leo Agosti 23, 2023 wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya mabingwa hao wa muda wote wa Tanzania utakaopigwa katika Dimba la Chamazi.

"Viungo wa Yanga, Mudathiri na Maxi ndio wachezaji hatari zaidi kwenye kikosi cha Yanga kwa sababu ya aina za pasi ambazo wanapiga kwenye half spaces kuhakikisha mastraika wao wanapata nafasi za kufunga.

"Hao ni wachezaji hatari sana, tutaingia kwa tahadhari kuwakabili," amesema Kocha Abdihamid Moalin.

Katika mechi ya Yanga dhidi ya ASAS Mudathiri alipiga pasi ya goli lililofungwa na Kennedy Musonda huku Maxi Mpia akipiga pasi iliyokwenda kwa Lomalisa ambaye alipiga pasi ya goli kwa Aziz Ki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live