Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawa ndiyop mastaa wa kike Bongo wanaosakata kabumbu nje

Clara Luvanga Ubingwa Hawa ndiyop mastaa wa kike Bongo wanaosakata kabumbu nje

Wed, 11 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi ya Wanasoka wa Soka la kulipwa Kimataifa kwa upande wa soka la Wanawake wazawa kutokea vilabu vya ndani nchini Tanzania inazidi kuongezeka kwa kasi ya kipekee.

Kama mwenendo huu ukiwa mzuri zaidi kwa muongo mmoja ujao Tanzania inatarajiwa kuwa miongoni mwa Mataifa yatayotoa wachezaji wengi wa kike katika kuliwakilisha Taifa kwenye Vilabu vinavyoshiriki Ligi kubwa Duniani.

Hawa hapa ni Wachezaji ambao kwa sasa wanakipiga mnamo vilabu vya Soka za Ligi za nje 2024;

Aisha Khamis Masaka anachezea Brighton& Hove Albion - Uingereza

Diana Lucas Msemwa anachezea Trabzonspor - Uturuki

Noela Patrick Luhala anachezea Tek Aviv University Club - Israel

Opah Clement Tukumbuke anachezea Henan FC - China

Hasnath Linus Ubamba anachezea Tutankhamun FC - Misri

Maimuna Hamis Kaimu anachezea FC Masr - Misri

Clara Cleitus Luvanga anachezea Al Nassr - Saudi Arabia

Suzana Adam Manumbu anachezea Tutankhamun FC - Misri

Julitha Singano anachezea FC JUAREZ - Mexico

Enekia Kasonga Lunyamila anachezea Mazatlanfemenil - Mexico.

Yupi historia yake ya Soka inakuvutia zaidi kati yao?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live