Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawa ndio wakali wa rekodi Mapinduzi

BOCCO 1140x640 Nahodha wa Simba John Bocco

Thu, 29 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mastaa wa Simba ndio wanaoonekana malejendi kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, awamu hii itakuwa inafanyika mara ya 17, zikishiriki timu mbalimbali.

Mashindano hayo yalianzishwa mwaka 2007, ambao mabingwa wa michuano hiyo, kinara akiwa Azam FC imechukua (5) Simba (nne), Yanga ( mbili), Mtibwa Sugar (mbili), wakati mwenyeji Miembeni ya Zanzibar (moja), URA (moja) na KCCA (moja).

Katika mashindano ya msimu huu jumla ya timu 12 zitachuana, zikiwa kwenye makundi manne, Kundi A likiwa na timu za Azam FC ya Dar es Salaam, Malindi na Jamhuri. Kundi B kuna klabu za Yanga na Singida Big Stars za Tanzania Bara na KMKM, kundi C kuna Simba, Mlandege na KVZ.

Kundi D, kuna timu ya Namungo ya Dar es Salaam, Aigle Noir ya Burundi na KVZ, ambapo kila kundi litatoa timu mbili za kucheza hatua na nusu fainali kabla ya kupatikana za kucheza fainali itakayopigwa Ijumaa ya Januari 13, 2017.

Mwanaspoti limefanya utafiti wake limegundua kuna wachezaji kutoka timu mbalimbali ambao wanastahili kupewa heshima kwenye michuano hiyo kwa kucheza kwa miaka mingi.

JOHN BOCCO - SIMBA

Bocco aliipandisha Azam Ligi Kuu mwaka 2008 na alibeba makombe mfululizo 2015, 2016 na 2017, Mapinduzi Cup 2016. Mwaka 2017 alijiunga Simba alikobeba makombe ya ligi mara tatu mfululizo 2017-2018, 2018-2019 na 2019-2020.

Wakati yupo Azam FC, Bocco aliisaidia timu hiyo kunyakua ubingwa wa Kombe la Mapinduzi 2012, 2013, 2017, huko akiwa na Simba kachukua mara moja akiwa nahodha 2022.

AISHI MANULA - SIMBA

Kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula naye kachukua ubingwa wa kombe hilo mara nne, akiwa na Azam kachukua mara tatu 2012, 2013, 2017 kwa Simba kaisaidia kuchukua mara moja mwaka 2022 na alikuwa kipa bora wa mashindano.

AGGREY MORRIS - AZAM

Beki wa Azam FC, Aggrey Morris kaisaidia timu yake kunyakua taji la ubingwa wa kombe hilo mara tano 2012, 2013, 2017, 2018 na 2019, timu yake ikiwa kinara wa mataji kwenye michuano hiyo.

SALUM ABUBAKARI ‘SURE BOY’ - YANGA

Kabla ya kujiunga na Yanga msimu uliopita, akiwa na Azam FC aliyopanda nayo daraja mwaka 2008, amechukua ubingwa wa Mapinduzi mara tano, 2012, 2013, 2017, 2018 na 2019.

ERASTO NYONI - SIMBA

Kiraka wa Simba, Erasto Nyoni, anayetajwa kwa nidhamu nzuri kwenye kazi hiyo, ukiachana na mataji matatu aliyochukua mawili akiwa Azam FC na moja Simba, ni kati ya wachezaji wakongwe kwenye michuano hiyo.

SHOMARI KAPOMBE - SIMBA

Beki wa Simba, Shomari Kapombe naye ni kati ya mastaa ambao waliyocheza kwa muda mrefu michuano hiyo, akiwa Simba na Yanga na kote alizisaidia timu hizo kutwaa mataji.

Mastaa wengine ambao wanauzoefu na mashindano hayo ni pamoja na kiungo wa Simba Jonas Mkude, ambaye sasa amekosa namba kikosi cha kwanza chini ya kocha Juma Mgunda, ametwaa taji hilo mara nne.

Meddie Kagere ambaye ndiye aliibuka mfungaji bora wa mashindano hayo akiwa na Simba baada ya kuifungia mabao matatu mwaka jana sasa ametimkia Singida United akiungana na Deus Kaseke, Ibrahim Ajibu na Said Ndemla wote wakiwa wameshashiriki mashindano hayo wakiwa nje ya timu hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti