Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawa ndio wabaya wa Yanga mechi ya Derby

Dabi Pic Data Mechi iilisha kwa sare huku Onyango akimdhibiti vyema Mayele

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya ngoma ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga kumalizika kwa suluhu, nyota wa Yanga, Yacouba Songne aliwataja mabeki wa Simba, Henock Inonga na Joash Onyango kuwa chanzo cha matokeo yale.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Yacouba alikuwa jukwaani akishuhudia mechi bila kuwa sehemu ya mchezo kutokana na kuuguza majeraha ya goti.

Baada ya mechi kumalizika bila bao, Mwanaspoti lilipiga stori na Yacouba ambaye aliuchambua mchezo kwa ujumla na kuwataja Inonga na Onyango.

“Ilikuwa mechi bora kwa pande zote mbili, Yanga ilicheza mpira wake wa kila siku, ilimiliki mpira katika vipindi vyote lakini ilishindwa kufunga kutokana na safu ya ulinzi ya Simba kuwa imara,” alisema Yacouba na kuongeza;

Mabeki wa kati wa Simba, Inonga na Onyango walicheza vizuri sana, walikuwa wakisambaratisha kila mipango ya Yanga na mechi kuisha kwa sare, alisema Yacouba ambaye ni raia wa Burkina Faso.

Yacouba alizungumzia pia majeraha yake na kufunguka kuwa siku si nyingi atarejea uwanjani.

“Nilitamani kuwepo kwenye mechi hii lakini ndio hivyo nina majeraha, nashukuru matibabu yalifanyika vizuri na sasa naendelea vizuri chini ya uangalizi wa daktari, siku si nyingi nitarejea.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live